1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI:Kiongozi wa wapiganaji wa kiislam cnhini Somalia ajisalimisha

22 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCYs

Mmoja wa viongozi wa ngazi ya juu wa wapiganaji wa muungano wa mahakama za kiislam nchini Somalia amejisalimisha kwa Marekani na serikali ya Kenya.

Maafisa usalama wa Kenya wamesema kuwa Sheikh Sharif Sheik Ahmed aliingia nchini Kenya na moja kwa moja akapelekwa mjini Nairobi ambako yuko chini uangalizi wa maafisa wa Marekani.

Ubalozi wa Marekani nchini Kenya ulikataa moja kwa moja kuthibitisha juu ya habari hizo.

Kiongozi huyo alikimbia Somalia akihofia usalama wake baada kutokuwa na msimamo kama wa wenzake.

Balozi wa Marekani nchini Michael Renneberger amekuwa akimuelezea Sheikh Sharrif Ahmed kuwa ni mtu mwenye msimamo wa wastani na anastahili kuwemo katika maridhiano ya kitaifa nchini Somalia.

Wakati huo huo Malawi imesema kuwa iko tayari kutuma kikosi cha askari katika jeshi la Umoja wa Afrika la kulinda amani nchini Somalia.

Waziri wa Ulinzi wa Malawi Davies Katsonga akizungumza mjini Nairobi hata hivyo amesema,bado nchi yake haijaamua idadi ya askari itakaotoa.

Hapo siku ya Ijumaa Umoja wa Afrika uliridhia kupelekwa kwa kikosi cha askari elfu 8 wa umoja huo nchini Somalia, kuchukua nafasi ya majeshi ya Ethiopea yanayotarajiwa kuondoka katika wiki chache zijazo.