NAIROBI: Watu watatu wauwawa kwenye ajali ya ndege | Habari za Ulimwengu | DW | 04.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NAIROBI: Watu watatu wauwawa kwenye ajali ya ndege

Watu watatu waliuwawa jana wakati ndege waliyokuwa wakisafiria ilipoanguka kwenye milima ya Loita ikiwa njiani kutoka mjini Nairobi ikielekea mbuga ya wanyama ya Masai Mara.

Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya safari ya Journeys by Design, iliyoandaa safari hiyo, Will Jones, amesema abiria wawili Wajerumani waliokuwa wakiishi nchini Uswisi na rubani mmoja raia wa Kenya, waliuwawa kwenye ajali hiyo.

Mkurugenzi huyo alitarajiwa kuwasili mjini Nairobi hapo jana kufuatilia ajali hiyo.

Barabara kutoka Nairobi kwenda Masai mara iko katika hali mbaya na watalii wengi hupendelea kusafiri kwa njia ya ndege badala ya kutumia magari.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com