NAIROBI: wanne wauwawa katika mtaa wa mabanda | Habari za Ulimwengu | DW | 28.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NAIROBI: wanne wauwawa katika mtaa wa mabanda

Watu waliokuwa na bunduki wamewauwa watu wanne katika eneo la mabanda jijini Nairobi.

Mauaji hayo yamezusha taharuki miongoni mwa raia na kudhaniwa kwamba huenda kundi haramu la Mungiki linalolaumiwa kwa mauaji kadhaa kuwa limehusika na mauaji hayo.

Kamanda wa polisi wa Kibera Herbert Khaemba amesema kwamba watu hao waliokuwa na bunduki walivamia sehemu hiyo ya makaazi ya mabanda yenye takriban wakaazi laki nane.

Watu hao walimwibia mtu mmoja ambae alipiga kelele kutaka usaidizi lakini majambazi hao walitoa bunduki na kumuuwa papo hapo.

Watu watatu waliojeruhiwa katika mkasa huo wamelazwa katika hospitali kuu ya Kenyatta jijini Nairobi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com