NAIROBI: Waislamu waandamana nchini Kenya | Habari za Ulimwengu | DW | 31.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NAIROBI: Waislamu waandamana nchini Kenya

Waislamu nchini Kenya waliandamana mbele ya makao makuu ya polisi mjini Nairobi siku ya Alkhamisi. Waandamanaji hao walikuwa wakilalamika dhidi ya kile walichosema ni kuzuiliwa na kuteswa kwa waislamu wenzao kinyume na sheria,katika hatua ya kupambana na ugaidi ambayo inahimizwa na Marekani.Kwa mujibu wa makundi yanayogombea haki za binadamu,serikali ya Kenya kwa siri imesafirisha Ethiopia washukiwa ugaidi wapatao darzeni kadhaa, kuhojiwa na maafisa wa Kimarekani nchini Ethiopia.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com