1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI : Serikali kupiga vita ukahaba wa watoto

29 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBnO

Serikali ya Kenya itafunga mahoteli ambayo yanaendekeza unyonyaji wa ngono kwa watoto unaofanywa na wageni na wenyeji tabia ambayo imeenea katika mkoa wa pwani nchini humo.

Waziri wa Sheria na masuala ya Katiba Martha Karua amesema serikali haitosita kuzipokonya leseni hoteli zinazongundulikana kuhusika na uovu huo.

Akiwahutubia wenye mahoteli katika mji wa mwambao wa Mombasa hapo jana usiku Karua amewataka wananchi kurepoti watuhumiwa kwa vile serikali imeandaa muswada ambao utawabana zaidi wakosaji.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF takriban asilimia 30 ya wasichana wa Kenya wenye umri kati ya miaka 12 na 18 katika mkoa wa pwani hujihusisha na utalii wa ngono tabia ambayo huchangia kueneza virusi vya HIV NA UKIMWI.