NAIROBI: Mwanamke kugombea uchaguzi wa rais Kenya
16 Novemba 2007Matangazo
Tume ya Uchaguzi nchini Kenya imewaruhusu wagombea 9 kushiriki katika uchaguzi wa rais utakaofanywa Desemba 27.
Mwanamke mmoja ni miongoni mwao.Wagombea wengine 4 wamekataliwa.Mbali na Rais Kibaki hata waziri wa nje wa zamani Musyoka na kiongozi wa upinzani Odinga watagombea uchaguzi huo.