1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NAIROBI: Moi ateuliwa kuwa mjumbe maalumu wa Sudan

Rais Mwai Kibaki wa Kenya amemteua rais mstaafu Daniel Torotoich arap Moi kuwa mjumbe maalumu wa amani nchini Sudan. Moi atakuwa na kibarua cha kusadia kuendeleza mpango wa amani katika eneo la kusini mwa Sudan ambako Kenya ina maslahi makubwa ya kiuchumi.

Rais Mwai Kibaki amemteua Daniel arap Moi baada ya kushauriana na rais wa Sudan, Omar Hassan al Bashir.

Ingawa Moi alijiuzulu katika maswala ya siasa mnamo mwaka wa 2002 baada ya kuitawala Kenya kwa miaka 24, kwenye utawala uliogubikwa na mateso dhidi ya viongozi wa upinzani na ufisadi uliotishia kuuvuruga uchumi wa nchi hiyo, kiongozi huyo wa zamani anaangaliwa kama mmoja wa wanasiasa waliokamaa barani Afrika.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com