1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NAIROBI : Kibaki avunja bunge tayari kwa uchaguzi

Rais Mwai Kibaki wa Kenya amelivunja bunge leo hii tayari kwa kile kinachoonekana kuwa uchaguzi mkali katika nchi hiyo yenye nguvu kubwa za kiuchumi Afrika Mashariki.

Kibaki amesema kwenye televisheni kwamba analivunja bunge hilo la tisa la Jamhuri ya Kenya kwa mujibu wa katiba mara moja.

Tume ya uchaguzi ya Kenya inatarajiwa katika kipindi cha siku 10 kutangaza tarehe ya uchaguzi ambayo inategemewa kuwa mwezi wa Desemba.

Kibaki anataraji kunyakuwa kipindi cha pili lakini uchunguzi wa maoni unaonyesha kuwa yuko nyuma ya mgombea wa upinzani na mshirika wake wa zamani Raila Odinga ambaye anaongoza kwa kati ya asilimia 43 na 52 dhidi ya asilimia 31 hadi 38 kwa Kibaki.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com