1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI : Itifaki ya Kyoto kuchambuliwa upya

18 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCrg

Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya hali ya hewa umemalizika katika mji mkuu wa Kenya Nairobi hapo jana kwa makubaliano ya kuchambuwa upya vifungu vya Itifaki ya Kyoto hapo mwaka 2008.

Itifaki ya Koyoto muda wake unatarajiwa kumalizika hapo mwaka 2012.Makundi ya mazingira kama vile Green peace na Marafiki wa Dunia pamoja na baadhi ya wajumbe wa Afrika wameelezea kukatishwa tamaa kwao kwamba mazungumzo hayo ya wiki mbili yameshindwa kufanikisha mambo mengi.

Mawaziri wa mazingira waliohudhuria mkutano huo akiwemo waziri wa mazingira wa Ujerumani Sigmar Gabriel pia wamekubali kuzishajiisha nchi za kitajiri kusaidia kugharamia upunguzaji wa utowaji wa gesi zenye kuathiri mazingira barani Afrika.