1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI: Gideon Moi akanusha ripoti kuhusu ubadhilifu

1 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBTk

Mwana wa kiume wa rais wa zamani wa Kenya,Daniel Arap Moi amekanusha ripoti ya mwaka 2004 iliyofichuliwa.Ripoti hiyo imesema,watu walio karibu na baba yake,waliiba pesa za serikali zipatazo Dola bilioni mbili.

Gideon Moi amenukuliwa na gazeti la Nairobi Star akisema kuwa atalishtaki gazeti la Uingereza,The Guardian-ambalo siku ya Ijumaa lilisema,kampuni moja ya ushauri ya kundi la Kroll,imefichua idadi kadhaa ya makampuni yaliyokuwa yakitumiwa na familia ya Moi na washirika wao,kupeleka pesa nchi za nje.

Siku ya Ijumaa,msemaji wa serikali aliipuza ripoti ya Guardian kuwa ni mbinu ya kisiasa dhidi ya Rais Mwai Kibaki ambae siku chache zilizopita aliungwa mkono hadharani na Moi kuchaguliwa tena.