1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAHR AL-BARED:Wafanyikazi 2 wa Msalaba mwekundu wauawa

11 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBsi

Wafanyikazi wawili wa Shirika la Misaada la Msalaba Mwekundu wameuawa hii leo baada ya kulengwa na risasi nje ya kambi ya wakimbizi kaskazini mwa Lebanon.Jeshi la Lebanon linapambana na wapiganaji wa kiislamu wanaojificha kwenye kambi hiyo.Wafanyikazi hao walipoteza maisha yao kwenye mlango wa kaskazini wa Nahr al Bared kwa mujibu wa maafisa wa Shirika la Msalaba Mwekundu.

Jeshi la Lebanon linaendelea kushambulia maeneo yanayoshukiwa kuwa maficho ya wapiganaji wanaohusika na Al Qaeda.Mapigano hayo mapya yanatokea siku moja baada ya mapigano makali tangu Juni mosi wakati jeshi la Lebanon lilipoanzisha operesheni ya kuwafurusha wapiganaji wa Fatah al Islam.

Kulingana na afisa wa ngazi za juu wa kijeshi mpaka sasa wanajeshi 11 wamepoteza maisha yao.Serikali ya Lebanon inatia juhudi za kufanya majadiliano kuhusu suala hilo.

Ahmad Fatfat ni waziri wa mambo ya ndani wa Lebanon