NAHR AL-BARED:Majeshi yaimarisha doria Nahr al Bared | Habari za Ulimwengu | DW | 01.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NAHR AL-BARED:Majeshi yaimarisha doria Nahr al Bared

Majeshi ya Lebanon yaliyojihami kwa silaha yalikaza kamba nje ya kambi ya wakimbizi wa Kipalestina ambako wapiganaji wa kiislamu wa Fatah al Islam wanaripotiwa kujificha.Hali katika kambi hiyo inaripotiwa kuwa mbaya huku moshi ulionekana ukifuka baada ya makombora kurushwa na jeshi yaliyolenga wapiganaji wa kiislamu katika kambi ya Nahr al Bared.

Kwa mujibu wa duru za kijeshi kundi la wanajeshi yapata alfu moja walihusika katika operesheni hiyo.

Serikali ya Lebanon kwa upande wake inashikilia kuwa kundi hilo la wapiganaji la Fatah al Islam liwafikishe wapiganaji wake kuhukumiwa baada ya kuhusika katika mashambulizi ya mwaka 75 hadi 90 wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Fatah al Islam wanasisitiza kuwa hakuna mpiganaji wao yoyote atakayehukumiwa.

Wakati huohuo Baraza la Usalaama la Umoja wa Mataifa limeidhinisha kuundwa kwa mahakama maalum kuwahukumu watuhumiwa wa mauaji ya marehemu Waziri mkuu Rafiq Hariri yaliyotokea mwaka 2005 katika shambulio la bomu.Nchi jirani ya Syria inalaumiwa kutekeleza mauaji ya kiongozi huyo wa zamani na mengine.Syria kwa upande wake inashukilia kuwa haijahusika na kushikilia kuwa haitashirikiana na mahakama hiyo mpya.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com