NAHR AL BARED : Jeshi lashambulia kambi ya wakimbizi | Habari za Ulimwengu | DW | 14.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NAHR AL BARED : Jeshi lashambulia kambi ya wakimbizi

Vikosi vya Lebanon vimeshambulia kambi ya wakimbizi wa Kipalestina kaskazini mwa Lebanon leo hii ambapo wanamgambo wanaochochewa na kundi la Al Qaeda waliojichimbia kwenye kambi hiyo wamefyatuwa maroketi manane aina ya Katyusha.

Jeshi na wanamgambo hao wa kundi la Fatah al Islam wamekuwa wakipambana vikali katika kambi hiyo ya Nahr al Bared kwa karibu wiki nane huku kukiwa hakuna dalili kwamba wanamgambo hao wa Kiislam wataitikia wito wa kusalimu amri.

Mapigano hayo yameuwa takriban watu 219 toketa tarehe 20 Mei ambapo vifo vya askari pekee ni zaidi ya 100 na kuvifanya vita hivyo kuwa vibaya kabisa kuwahi kushuhudiwa ndani ya nchi tokea vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Lebanone vya mwaka 1975 hadi mwaka 1990.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com