Nahodha wa Fiorentina afariki dunia
5 Machi 2018
Tuanze na tanzia: Nahodha wa klabu ya Fiorentina na mchezaji wa timu ya taif ya Italia Davide Astori amefariki kutoka na ugonjwa wa ghafla akiwa na umri wa miaka 31 jana Jumapili , na kuliacha soka la Italia katika mshituko mkubwa.
Ligi ya Serie A iliahirisha michezo yote ya jana , ikiwa ni pamoja na pambano la watani wa jadi kati ya AC Milan na Inter Milan, wakati vilabu vya Italia na Ulaya kwa jumla na wachezaji kadhaa walituma salamu zao za rambi rambi na kueleza mshangao wao kwa kifo hicho cha ghafla. Mlinzi Astori , akiwa katika msimu wake wa 10 katika Serie A, alikutwa amefariki katika chumba alichopanga hotelini mjini Udine, ambako Fiorentina ilikuwa ipambane na Udinese katika uwanja wa Dacia Arena jana Jumapili. Astori, ambaye ameshiriki michezo 298 katika Serie A , alijiunga na Fiorentina kwa mkopo mwezi Agosti mwaka 2015 na klabu hiyo ilimsaini moja kwa moja mwaka mmoja baadaye. Aliichezea Cagliari kwa misimu sita na mwaka mmoja kwa mkopo katika klabu ya AS roma. Mungu aieweke roho ya marehemu mahali pema , ameen.
Mwandishi: Sekione Kitojo / dpae / rtre / afpe
Mhariri: Yusuf Saumu