1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NABLUS:Amri ya kutotoka nje yatekelezwa Ukingo wa Magharibi

26 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCOR

Wapalestina 30 elfu wanaoishi katika ukingo wa Magharibi wametakiwa kubakia majumbani mwao kufuatioa amri ya kutotoka nje iliyowekwa na wanajeshi wa Israel waliovamia mji wa Nablus.

Katika uvamizi huo watu 30 walikamatwa huku wanajeshi wawili wa kiisraeli wakiuwawa kwenye mripuko wa bomu.

Hatua ya kuvamia mji huo ilichukuliwa baada ya kugunduliwa hapo jumamosi mahabara ya miripuko katika mji huo.

Kwengineko katika ukanda wa Gaza takriban wapalestina wanne wameuwawa na wengine 20 kujeruhiwa katika mapigano mapya baina ya makundi ya wafuasi wa chama cha Hamas na Fatah.

Hayo ndio mapigano makali kuwahi kutokea kati ya makundi hayo tangu pande hizo mbili kukubaliana kuunda serikali ya umoja wa kitaifa wiki tatu zilizopita.