NABLUS: Mwanamgambo wa kipalestina auwawa | Habari za Ulimwengu | DW | 19.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NABLUS: Mwanamgambo wa kipalestina auwawa

Wanajeshi wa Israel wamemuua mwanamgambo wa kipalestina mjini Nablus huko Ukingo wa Magaribi aliyekuwa akisakwa kwa kipindi kirefu. Jeshi la Israel linasema vikosi vyake viliitambua gari iliyokuwa imewabeba watu watatu waliokuwa wakisakwa na kuizingira.

Baadaye walifyatua risasi wakati wanaume hao walipojaribu kutoroka. Imeripotiwa kwamba mwanamume aliyeuwawa ni mwanachama wa kundi la wanamgambo la Al Aqsa.

Duru za jeshi zinasema wanaume wengine wawili walijeruhiwa na kupelekwa katika hospitali ya jeshi la Israel.

Wanaume wote watatu wanatuhumiwa kuhusika katika kuwasajili washambuliaji wa kujitoa muhanga maisha na kupanga mashambulio dhidi ya waisraeli.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com