1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mzozo wa takataka wasababisha jeshi kuingilia kati Italy

7 Januari 2008
https://p.dw.com/p/ClYN

NAPLES:

Jeshi la Italy limeombwa kusaidia kuzoa takataka za tani zaidi ya laki tano ambazo zimeundika katika mji wa kusini mwa nchi hiyo wa Naples.

Wakazi wa kitongoji kimoja wameweka vizuizi barabani wakipinga kufunguliwa tena kwa sehemu moja ya jalala iliofungwa miaka 11 iliopita kutokana na sababu za kiafya.

Waziri Mkuu Romano Prodi ameamua shule kufunguliwa licha ya hofu kuwa takataka hizo zaweza kusababisha magonjwa. Mgogoro wa sasa wa taka mjini Naples ulianza wiki mbili zilizopita wakati magari ya kuzolea takataka yalisimamishwa kufanya kazi kwa kuwa maeneo yote ya kumwaga takataka hizo kujaa.