Mzozo wa kisiasa nchini Georgia | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 08.11.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Mzozo wa kisiasa nchini Georgia

Serikali ya Tblisi yatangaza sheria ya hali ya hatari nba kuituhumu Urusi kua nyuma ya machafuko

Polisi wapambana na waandamanaji mjini Tblisi

Polisi wapambana na waandamanaji mjini Tblisi

Rais Mikhail Saakachvili wa Georgia ametangaza sheria ya hali ya hatari itakayoendelea kwa muda wa siku 15,baada ya kuituhumu Urusi kuwa nyuma ya wimbi la maandamano ya upamnde cwa upinzani linaloikumba nchi hiyo.

Kuna Njama ya kufanya mapinduzi na kuleta vurugu nchini” amesema hayo waziri mkuu Zourab Nogaideli kupitia televisheni ya taifa huku waziri wake wa maendeleo ya kiuchumi Geogry Arveladze akitangaza kufungwa matangazo yote ya televisheni za kibinafsi hadi sheria ya hali ya hatari itakapobatilishwa.

Jumuia ya kujihami ya magharibi NATO imelaani uamuzi wa serikali ya Georgia wa kutangaza sheria ya hali ya hatari.”NATO inafuatilizia kwa wasi wasi mkubwa hali namna ilivyo nchini Georgia” amesema hayo katibu mkuu wa jumuia hiyo Jaap de Hoop Scheffer katika taarifa iliyotangazwa mjini Brussels hii leo.

Hali ya hatari imetangazwa kupitia siku sita za malalamiko ya umma unaomtaka rais Saakachvili ajiuzulu.Anakosolewa na upande wa upinzani kutumia vibaya mali ya umma na kuziendeya kinyume haki za binaadam.

Waziri wa zamani wa mambo ya nchi za nje wa Georgia Salome ZURBISHVILI anamtaja rais Mikhail Saakachvili kua ni muimla wa kibolsheviki.

“Nnadhani tunajua vyema demokrasia manaake ni nini na tunawataka marafiki wa Georgia wasalie kua marafiki wa Georgia na sio marafiki wa Saakashvili.Tumejionea wenyewe kumbe yeye ni muimla wa kibolsheviki.”

Viongozi wa Georgia wanadai waandamanaji wanachochewa kutoka nje.

Katika hotuba yake kwa njia ya televisheni baada ya vikosi vya usalama kutumia nguvu kuwatawanya waandamanaji, rais Saakachvili alisema hapo awali Georgia inakumbwa na kitisho kikubwa cha wafanya fujo.

“Maafisa wa ngazi ya juu kutoka idara maalum za Urusi wanabeba dhamana ya hali hii” amesema rais Saakachvili akiongeza kusema tunanukuu”ushahidi upo-“Mwisho wa kumnukuu.

Serikali ya Georgia imewafukuza wanadiplomasia watatu wa Urusi.

Urusi imekanusha tuhuma zaa kua nyuma ya maandamano ya upande wa upinzani nchini Georgia na kuitaka jumuia ya kimataifa iingilie kati .

“Tunaamini jumuia ya kimataifa,mashirika makuu ya haki za binaadam,Umoja wa mataifa,baraza la ulaya na jumuia ya usalama na ushirikiano barani Ulaya yanabidi yaingilie kati kuitaka Georgia ikomeshe matumizi ya nguvu,iheshimu kikamailifu haki za binaadam na isake ufumbuzi wa matatizo ya ndani ya kisiasa kwa kuheshimu katiba,bila ya matumizi ya nguvu” amesema hayo Mikhael Kamynine ambae ni msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za nje ya Urusi.

Serikali ya Urusi imemwita muambata wa Georgia kuamrifu hatua zinazopangwa kuchukuliwa kujibu uamuzi wa Tblisi wa kuwafukuza wanadiplomasia wake watatu.Habari za hivi punde zinasema Moscow imewafukuza wanadiploamsia watatu wa Georgia kama jibu kwa uamuzi kama huo uliopitishwa jana na serikali ya Georgia.

 • Tarehe 08.11.2007
 • Mwandishi Oummilkheir
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/C776
 • Tarehe 08.11.2007
 • Mwandishi Oummilkheir
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/C776

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com