Mzozo ndani ya chama cha wananchi CUF Tanzania
12 Desemba 2011Matangazo
Mbunge wa chama hicho kutoka Wawi, Pemba, Hamad Rashid Mohamed, ameulaumu vikali uongozi na mwenendo wa chama hicho, akisema katibu mkuu wa chama, Maalim Seif Shariff Hamad, ambaye pia ni makamo wa kwanza wa rais wa Zanzibar, inafaa aache dhamana ya ukatibu mkuu wa chama. Duru za wachambuzi wa mambo zinasema mwenyewe Rashid Hamad Mohammed anafanya kampeni ya kuwashawishi wanachama wa chama cha CUF wamchague yeye kuwa katibu mkuu.
Kupata zaidi juu ya mfarakano huu katika uongozi wa CUF, Othman Miraji alizungumza na makamo wa katibu mkuu wa CUF, upande wa Visiwani Zanzibar, ambaye pia ni mwakilishi wa mji mkongwe, Ismail Jussa. Alisimulia hivi kuhusu mkasa huo..
Mwandishi: Othman Miraji
Mhariri: Mohamed Abdulrahman