1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwimbaji maarufu Luciano Pavarotti aaga dunia

Maja Dreyer6 Septemba 2007

Leo asubuhi, mwimbaji maarufu sasa alikuwa na sauti ya Tenor, sauti ya juu ya kiume, Luciano Pavarotti alifariki dunia katika nyumba yake mjini Modena, Italia, akiwa na umri wa miaka 71.

https://p.dw.com/p/CHjQ
Luciano Pavarotti
Luciano PavarottiPicha: AP

Risala za rambirambi zontolewa toka kote ulimwenguni akiwemo Ban Ki Moon, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, waimbaji maarufu kama Placido Domingo, Jose Carreras au Elton John pamoja na rais na mawaziri mkuu wa nchi mbali mbali. Bw. Pavarotti alijulikana kama mmoja kati ya mwimbaji wazuri zaidi wa Tenor katika kizazi chake.

Tangu miaka kadhaa iliyopita, mwimbaji Luciano Pavarotti alipambana na ugonjwa wa kansa. Katika tamasha zake za mwisho alitazamika kuketi wakati wa kuimba badala ya kusimama. Lakini hata alipojua kwamba ana kansa ya kongosho (pancreas), Pavarotti alisisitiza mara kwa mara kuwa alikuwa na maisha mazuri na ya furaha. Hasa ni mashabiki wake ambao walimfurahisha zaidi na kumshawishi kuimba jukwaani hadi mwisho.

Luciano Pavarotti amesema: “Ni kukumbuka, unajua kwenye kazi yetu kuna makumbusho mengi. Na ikiwa umefanikiwa maishani, makumbusho ni mazuri. Kwangu mimi nimefurahia zaidi kukutana na watu wa kawaida, hususan katika nchi na kigeni ambapo nilifahamu kuwa mimi ni ishara ya taifa la Italy. Nafikiri ndiyo hiyo inayotofautisha kazi yetu na kazi nyingine.”

Alikuwa ni baba yake Luciano Pavarotti ambaye mwenyewe alipenda sasa kuimba na kumfanya mtoto wake kupenda muziki ya opera. Mwaka 1961 Luciano alipata umaarufu pale aliposhinda katika mashindano ya kimataifa ya kuimba. Katika miaka iliyofuata alipanda majukwaa yote muhimu ya opera duniani kote. Vile vile Pavarotti hakuogopa kuimba muziki wa kisasa zaidi.

Barani Afrika pia Luciano Pavarotti ana mashabiki wengi, kama anavyothibitisha Bi Winnie Likhayo, mkuu wa shule ya muziki jijini Nairobi, Kenya.

Umaarufu wa Luciano Pavarotti ulizidi kuenea pale aliposhirikiana na waimbaji wengine wa Tenor Placido Domingo na Jose Carreras ambao walijulikana kama “The three Tenors”. Kwa pamoja waliimba wimbo wa mtungaji muziki Puccini ambao ulikuwa wimbo huu wa kombe la dunia la kandana lililofanyika nchini Italy mwaka 1990. Nakala Millioni 10 za tamasha hili ziliuzwa na kuifanya kuwa album maarufu zaidi ya muziki aina ya klassikali ambayo iliwahi kuwepo.

Mwimbaji Luciano Pavarotti alishiriki katika matamasha mengi ya kuchangia fedha kwa watu maskini duniani. Wimbo wa “Ave Maria” aliuimba katika burudani ya kuchanga pesa kwa watoto wahanga wa vita.