1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

ICC yaihimiza Israel na kundi la Hamas kuheshimu sheria

3 Desemba 2023

Mwendesha mashtaka mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) Karim Khan, ametoa wito kwa pande mbili zinazohusika katika vita kati ya Israel na Hamas kuzingatia sheria za kimataifa

https://p.dw.com/p/4Zj6f
Mwendesha mashtaka mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) Karim Khan, wakati wa mkutano na wanahabari mjini The Hague nchini Uholanzi mnamo Julai 3, 2023
Mwendesha mashtaka mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) - Karim KhanPicha: Peter Dejong/AP/picture alliance

Baada ya ziara ya siku nne katika eneo la Israel lililoshambuliwa na Hamas mnamo Oktoba 7 na katika eneo linalokaliwa kimabavu na Israel la Ukingo wa Magharibi, Khan amesema sheria ya kimataifa haita utata linapohusika suala la kufikisha msaada wa kiutu unakohitajika.

Khan amesema lazima raia wa Gaza wapate bidhaa za kimsingi

Khan amesema lazima raia wapate chakula, maji na vifaa vya matibabu vinavyohitajika kwa haraka na bila kucheleweshwa , na kuongeza kuwa kunapaswa kuwa na kasi na kwa kiwango cha kufanya hivyo.

Khan awaonya wadau kuhusu kuchukuwa hatua

Mwendesha mashtaka huyo wa ICC pia amesema kuwa kundi la Hamas halipaswi kutumia vibaya msaada huo.

Khan amewataka wadau wote kuzingatia sheria ya kimataifa ya kibinadamu na kuonya kuwa iwapo hawatafanya hivyo, hawapaswi kulalamika wakati ofisi yake itakapohitajika kuchukuwa hatua.