1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Afrika

Mwandishi wa Habari auwawa na Polisi mjini Mbeya

Uongozi wa Africa Media, ambao ni wamiliki wa kituo cha televisheni "Channel 10" Tanzania umelaani vikali mauwaji ya mwandishi wake Daudi Mwangosi.

Purukushani za polisi na chama cha upinzani Chadema

Purukushani za polisi na chama cha upinzani Chadema

Mwangosi aliuwawa kutokana na mripuko wa bomu wakati wa purukushani za polisi na wafuasi wa chama kikuu cha upinzani nchini humo CHADEMA zlizotokea katika ufunguzi wa matawi wa chama huko huko Mkoani Iringa. Kutoka Dar es salaam Sudi Mnette alizungumza na Mhariri Mkuu wa Habari, kituo cha Channel 10, Dina Chahali na kwanza alimuuliza kama mratibu wa habari, kifo cha mwandishi Mwangosi kimetokana na nini kwa ufahamu wake.

(Kusikiliza mazungumzo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)

Mwandishi:Sudi Mnette

Mhariri: Saumu Yusuf

Sauti na Vidio Kuhusu Mada