1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanamuziki Whitney Houston afariki

15 Februari 2012

Mwanamuziki mashuhuri wa Marekani Whitney Houston amefariki dunia. Polisi katika mji wa Los Angeles nchini Marekani wamesema Whitney (48), amekutwa amekufa katika hoteli ya Beverly Hills.

https://p.dw.com/p/143UK
File- In this Oct. 28, 2006, file photo, musician Whitney Houston arrives at the 17th Carousel of Hope Ball benefiting the Barbara Davis Center for Childhood Diabetes in Beverly Hills, Calif. Houston died Saturday, Feb. 11, 2012, she was 48. (Foto:Matt Sayles/AP/dapd)
Whitney HoustonPicha: dapd

Habari za kifo cha nyota huyo zimekuja wakati ulimwengu wa muziki ukijiandaa kwa sherehe za tuzo ya Grammy leo Jumapili, na pia saa chache kabla ya tafrija ya chakula kwenye hotel ambapo marehemu Whitney Houston amepatwa na mauti.

Afisa wake wa habari Kristen Foster ambaye alikuwa wa kwanza kutangaza kifo hicho hakuelezea chanzo cha kifo chake. Hata hivyo katika miaka ya hivi Karibuni mwanamuziki huyo amekuwa akisumbuliwa na athari za matumizi ya madawa ya kulevya.

Whitney Houston alijipatia Umaarufu mkubwa katika miaka ya 1980 na 1990, kwa nyimbo zilizovuma kama  ''How will I Know'', ''Saving all my Love for You'' na ''I will always Love You''. Alishiriki pia katika uwanja wa uigizaji na kuwa katika filamu mashuhuri ya ''Bodyguard''

Wakati wa umaarufu wake Whitney Houston alishinda tuzo sita za Grammy. Magwiji wa muziki wametoa rambi rambi zao kupitia mitandao ya kijamii, wakimueleza Bi Houston kama mtu ambaye hatasahaulika katika fani ya Muziki.

Kufuatia kifo hicho Sekione Kitoji wa DW alizungumza na mwanamuziki maarufu kutoka Tanzania Waziri Ali ambae alieleza kusikitishwa kwake.

Mwandishi Daniel Gakuba/RTRE

Mhariri Amina Abubakar