1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanamfalme Harry wa Uingereza apigana mstari wa mbele Afghanistan

29 Februari 2008
https://p.dw.com/p/DFfg

LONDON:

Wizara ya Ulinzi nchini Uingereza imethibitisha ripoti za vyombo vya habari kuwa Mwanamfalme Harry yupo Afghanistan tangu mwezi wa Desemba akipambana na wanamgambo wa Taliban.Kuambatana na makubaliano yaliyokuwepo pamoja na Wizara ya Ulinzi ya Uingereza,vyombo vya habari vilikubali kutoripoti juu ya kupelekwa kwa Mwanamfalme Harry nchini Afghanistan.Lakini siku ya Alkhamisi wizara hiyo ilithibitisha kuwa Mwanamfalme huyo yupo Afghanistan pamoja na vikosi vya Uingereza katika mstari wa mbele.Wizara ya Ulinzi ilichukua hatua hiyo baada ya tovuti za Kijerumani,Australia na Marekani kuripoti kuwa mwanamfalme Harry yupo Afghanistan.Sasa jeshi la Uingereza linafikiria upya kuhusu kuwepo kwa mwanamfalme huyo nchini Afghanistan.