Mwanahiti: zawadi ya Unyago Uzaramoni II
16 Mei 2012Mwanahiti wapo katika jamii nyingi kama vile Ghana, Nigeria na Ulaya. Hapa Ulaya eneo la Viena aligunduliwa Mwanahiti ambaye alitumiwa miaka mingi iliyopita.
Msanii mmoja wa Kizaramo alikuwa na kilio cha urithi kwa binti yake anasema maneno haya:
“…Kinachoniuma roho: Nikimtazama mwanagu Pili, anavyonitegemea
Huwa najiuliza sana, Kitu gani nitampa mwana?
Au nitapofariki, Mwanagu urithi gani nitamuachia?
Najua atapata tabu mama, hapa katika dunia
Jamani… Liwalo na liwe, hayo yameshatokea
Hakuna la kufanya, kuweza kuikoa
Liwalo na liwe, hayo yameshatokea…”
Basi kwa kuwa mwimbaji wa wimbo huo alikuwa mwanaume hakujua kuwa binti yake anao urithi wa heshima kubwa, Mwanahiti.
Mwandishi: Adeladius Makwega
Mhariri: Miraji Othman
Makala ya Utamaduni na Sanaa : Mwanahiti II