1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwafaka juu ya kugawana madaraka uko mbali kufikiwa nchini Kenya

16 Februari 2008

Mazungumzo ni mapana na magumu asema Kofi Annan

https://p.dw.com/p/D8O2

NAIROBI

Serikali ya Kenya na chama kikuu cha upinzani wamekubaliana kuunda tume huru ya kuchunguza mgogoro wa matokeo ya uchaguzi wa Desemba mwaka jana yaliyomrudisha madarakani rais Mwai Kibaki.

Katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan alitoa tangazo hilo baada ya kuongoza mazungumzo ya siku mbili juu ya suala hilo kati ya serikali na chama cha bwana Raila Odinga cha ODM.Aidha Kofi Annan alikiri kwamba masuala yanayozungumziwa ni mengi na magumu kufikia mwafaka lakini ana matuamini kwamba pande hizo mbili zinazozozana kuhusu madaraka zitaafikiana kuunda serikali ya mseto.Mazungumzo hayo ya suluhu yataanza tena jumanne ijayo baada ya Annan kukutana na rais Kibaki na bwana Odinga jumatatu.Matokeo ya uchaguzi wa rais hapo mwezi Desemba ambayo upinzani unasema yalikuwa ya uongo yalizusha mapigano makali ya kikabila na kusababisha kuuwawa kwa watu zaidi ya 1000 nchini Kenya na kuwaacha maelfu ya wengine bila makaazi.