Mvutano waibuka upya Sudan | Matukio ya Kisiasa | DW | 23.05.2011
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Mvutano waibuka upya Sudan

Tume ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa nchini Sudan, imetoa mwito kwa serikali ya Sudan kuviondoa vikosi vyake kutoka eneo la Abyei linalopakana na Sudan ya Kusini.

Karte Südsudan, Sudan, Khartum. DW-Grafik: Per Sander 2011_02_08_sudan_südsudan.psd

Ramani ya Sudan na Kusini ya Sudan

Katika taarifa iliyotolewa Khartoum, mji mkuu wa Sudan, wajumbe wa Baraza la Usalama, wameelezea wasiwasi wao kuhusu hali inayozidi kuwa mbaya katika eneo la Abyei. Siku ya Jumamosi, wanajeshi wa kaskazini walilidhibiti eneo hilo linalogombewa na Sudan ya Kaskazini na Kusini.Kura ya maoni iliyopangwa kufanywa mwezi wa Januari kuamua hatima ya eneo hilo la mpakani lenye utajiri wa mafuta, imeahirishwa kwa sababu ya hali ya mvutano na matatizo ya mipangilio.

Southern Sudanese celebrate the announcement of preliminary referendum results in the southern capital of Juba on Sunday, Jan. 30, 2011. Referendum officials indicated that nearly 99 percent of all voters cast ballots in favor of southern independence. Southern Sudan will remained united with the north until the expiration of Comprehensive Peace Agreement in July 2011 at which point it is set to emerge as a separate state. (AP Photo/Pete Muller)

Wasudan wa Kusini wafurahia matokeo ya kura ya maoni

Mwezi huo wa Januari, katika kura ya maoni iliyopigwa Sudan ya Kusini, wakaazi wake waliamua kujitenga na Kaskazini. Taifa huru la Sudan ya Kusini linatazamiwa kutangazwa rasmi tarehe 9 Julai, ikiwa ni miaka sita baada ya kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan.

 • Tarehe 23.05.2011
 • Mwandishi Martin,Prema/dpa,afp
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/RPOP
 • Tarehe 23.05.2011
 • Mwandishi Martin,Prema/dpa,afp
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/RPOP

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com