1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi wa Houthi washambuliwa Yemen

2 Novemba 2018

Muungano unaoongozwa na Saudi Arabia unaopambana na waasi nchini Yemen umesema umeushambulia uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Sanaa pamoja na kambi ya jeshi ilio karibu na uwanja huo zinazotumiwa na waasi wa Houthi.

https://p.dw.com/p/37YQQ
Saudi Arabischer F-15 Kampfjet
Picha: picture-alliance/AA/I. Erikan

Shambulizi hili limetokea siku moja baada ya serikali zinazouunga mkono muungano huo kujitolea kuanzisha tena mazungumzo ya amani na waasi hao.

Mapigano hayo yametokea siku kadhaa baada ya miito ya mara kwa mara kutoka Marekani ya kusimamisha mapigano yaliodumu miaka mitatu na nusu ambayo serikali zinazoiunga mkono Saudi Arabia zilisema ziko tayari kuunga mkono wito huo wa kusitisha mapigano.

Ein Stammesangehöriger, der den Houthi-Rebellen treu ist, hat während einer Versammlung Parolen gesungen, die darauf abzielten, mehr Kämpfer an Kampffronten zu mobilisieren, um in einigen jemenitischen Städten, in Sanaa, Jemen, Regierungstruppen zu bekämpfen
Baadhi ya waasi wa Houthi Picha: picture-alliance/H.Mohammed

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Jim Mattis na Waziri wa mambo ya nchi za nje Mike Pompeo wametoa wito wa kumalizika vita vya Yemen ikiwemo mashambulizi ya angani yanayotekelezwa na muungano huo.

Muungano wadai Sanaa inatumiwa kuwashambulia

Msemaji wa muungano huo kanali Turki al-Malki alikiambia kituo cha televisheni cha Saudi Arabia cha Al Ekhbaria kwamba, waasi wa Houthi wamekuwa wakitumia kambi ya kijeshi mjini Sanaa kuwashambulia kwa maroketi na makombora. Duru za kijeshi kutoka bandari ya Hodaida zimesema mapigano yalianza hii leo asubuhi huku  helikopta zikionekana angani.

Hata hivyo Dk. Hilal Khashan profesa wa siasa katika chuo kikuu cha Marekani mjini Beirut amesema Marekani kwa sasa inataka kumaliza vita nchini Yemen kutokana na kwamba vita hivyo havimnufaishi yeyote.

"Marekani mara azote ilitaka kumaliza vita nchini Yemen kwasababu inaamini vita hivyo havimfaidisho yoyote na wasaudi hawatashinda vita hivyo. Na kando na hayo vita vimesababisha ubaribifu mkubwa na vikiendelea raia wengi wa yemen wataumia," alisema Hilal Khashan.

USA PK vom Verteidugungsminister Jim Mattis im Pentagon
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Jim MattisPicha: Getty Images/Z. Gibson

Shinikizo la kurejea kwenye meza ya mazungumzo

Muungano huo unaoongozwa na Saudi Arabia uliweka majeshi yake karibu na mji huo siku ya Jumatano ikiwa ni hatua ya kuwashinikiza waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran kurejea katika mazungumzo ya amani yanayoongozwa na Umoja wa Mataifa.

Vikosi vilivyotiifu kwa muungano huo vimesema mashambulizi ya muungano yalishika kasi siku ya alhamisi usiku katika maeneo ya waasi ya Mashariki katika lango la kuingia kwenye mji huo wa bandari, ambayo ndio njia ya kuingia mji mkuu Sanaa na eneo la kusini.

Saudi Arabia, Marekani, Umoja wa falme za kiarabu na washirika wa kisunni wamekuwa wakipigana dhidi ya waasi wa Houthi tangu mwezi Machi mwaka 2015. Waasi hao wa Houthi wanaodhibiti eneo kubwa la kaskazini mwa Yemen ikiwemo mji mkuu sanaa walifanya serikali inayotambuliwa kimataifa kukimbilia uhamishoni mwaka 2014.

Mwandishi Amina Abubakar/Reuters/AFP

Mhariri: Yusuf Saumu