1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Musharraf ashinikizwa kujiuzulu

3 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CjmJ

ISLAMABAD

Yatahadharishwa kwamba Rais Pervez Mudharraf wa Pakistan ambaye ni mshirika wa Marekani lazima ajiuzulu kabla ya uchaguzi wa mwezi ujao venginevyo atahatarisha nchi yake kutumbukia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Tahadhari hiyo imetolewa leo hii na jopo mashuhuri la ushauri duniani pamoja na upinzani nchini Pakistan baada ya serikali kuahirisha uchaguzi wa bunge uliokuwa umepangwa kufanyika mwezi huu hadi tarehe 18 mwezi wa Februari kwa sababu ya machafuko yaliotokaana na kuuwawa kwa waziri wa mkuu wa zamani wa nchi hiyo Benazir Bhutto.

Chama cha upinzani cha waziri mkuu wa zamani Nawaz Sharif kimesema uchaguzi huru na wa haki hauwezi kufanyika chini ya utawala wa Musharraf.

Kundi la Kimataifa linaloshughulikia migogoro lenye makao yake mjini Brussels Ubelgiji limetaka Marekani itambuwe kwamba Musharraf ni mzigo mkubwa na venginevyo anajiuzulu hali ya mvutano itazidi kuwa mbaya na kwamba jumuiya ya kimataifa inaweza kukabiliwa na jinamizi la vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa taifa hilo linalomiliki silaha za nuklea.

Wakati huo huo wafuasi wa Benazir Bhutto leo wamesisitiza kwamba uchunguzi wa Umoja wa Mataifa ni njia pekee ya kubainisha ukweli juu ya mauaji yake na wametupilia mbali tangazo la serikali kwamba wapepelezi wa Scotland Yard wa Uingereza wa kupiga vita ugaidi watasaidia katika uchunguzi huo.