Munterfering an’gatuka siasa | Habari za Ulimwengu | DW | 22.11.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Munterfering an’gatuka siasa

Naibu Kansela wa Ujerumani anayeondoka madarakani Franz Munterfering ametowa wito kwa serikali ya mseto nchini kushirikiana kwa karibu zaidi.

Munterfering amesema ushirikiano wa vyama hivyo viwili vikuu vya kisiasa nchini cha Social Demnokratik na Christian Demokratik umechangia kuwepo kwa utamaduni wa kisiasa nchini Ujerumani.

Rais Horst Köhler amemuapisha Olaf Scholz kushika wadhifa wa Muntefering wa waziri wa kazi wakati waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmeir anachukuwa wadhifa wa naibu kansela.

Rais Köhler alimuaga rasmi Munterfering hapo jana mjini Berlin ambapo amemshukuru kwa mchango wa huduma aliotowa kwa wananchi wa Ujerumani na kumpongeza kwa hilo pamoja na kusema kwamba atakuwa anamkosa sana .

Franz Munterfering alijiuzulu kutoka serikalini hapo Novemba 13 ili kupata muda zaidi wa kumshughulikia mke wake ambaye ni mgonjwa.

 • Tarehe 22.11.2007
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CQGO
 • Tarehe 22.11.2007
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CQGO

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com