MUNICH: Huber achaguliwa mwenyekiti wa CSU | Habari za Ulimwengu | DW | 29.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MUNICH: Huber achaguliwa mwenyekiti wa CSU

Nchini Ujerumani,Waziri wa Uchumi wa Jimbo la Bavaria Erwin Huber amechaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa chama cha kifahidhina cha CSU. Alipohotubia mkutano wa CSU mjini Munich,Huber alisema,anaamini kuwa chama kinaweza kufanikiwa tu ikiwa kutakuwepo uaminifu na mshikamano badala ya kila mmoja kujiendea njia yake.Huber alie na miaka 61 amechaguliwa kwa wingi wa asilimia 58 kumrithi Edmund Stoiber.

Wadhifa huo uligombewa pia na Waziri wa Kilimo wa Ujerumani Horst Seehofer aliepata asilimia 39 ya kura.Mgombea mwengine Gabriele Pauli alipata asilimia 2 ya kura zilizopigwa katika mkutano maalum wa chama cha CSU mjini Munich.

Waziri wa Ndani wa Jimbo la Bavaria,Günther Beckstein anamrithi Stoiber kama waziri mkuu wa jimbo hilo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com