Muhammad Ali atibiwa homa ya mapafu
22 Desemba 2014Matangazo
Ali mwenye umri wa miaka 72, anaugua maradhi ya kiharusi, na msemaji wake Bob Gunnell amesema hali yake iko imara tangu alipolazwa katika hospitali moja nchini Marekani siku ya Jumamosi.
Ali aligunduliwa kuwa na kiharusi mnamo mwaka 1984, ikiwa ni miaka mitatu baada ya kustaafu kutoka ulingo wa masumbwi. Bondia huyo wa zamani alionekana hadharani mara ya mwisho mwezi Septemba katika mji wake wa nyumbani wa Louisville, kuhudhuria hafla ya utoaji wa tuzo za kibinaadamu za Muhammad Ali, lakini hakuzungumza.
Mwandishi. Bruce Amani/dpa
Mhariri. Gakuba Daniel