1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mubarak afikishwa mahakamani kwa mara ya pili

15 Agosti 2011

Rais alieondolewa madarakani nchini Misri, Hosni Mubarak amewasilishwa mahakamani mjini Cairo, akiwa katika machela kwa ajili ya kujibu mashitaka yake ya mauwaji na rushwa leo.

https://p.dw.com/p/12GgX
Rais wa zamani wa Misri, Hosni MubarakPicha: dapd

Kwa mujibu wa televisheni ya serikali ya Misri, kwanza Mubarak alisafirishwa kwa helikopta na baadaye akapakiwa katika gari la wagonjwa mpaka katika jengo la mahakama nchini humo.

Mubarak mwenye umri wa miaka 83, na ambaye aliwekwa kizuizini katika hospitali moja iliyopo mjini Cairo tangu kuonekana kwake siku ya kwanza Agosti 3 alioneshwa na televishini hiyo akitolewa katika gari la wagonjwa akiwa katika kitanda cha hospitali.

Ägypten Prozeß gegen Hosni Mubarak wird fortgesetzt in Kairo
Hosni Mubarak akiwa katika uzioPicha: dapd

Mubarak alikuwa akionekana kuzungumza maneno mawili matatu na wanawe Alaa na Gamal ambao nao watuhumiwa na mashitaka hayo.

Baada ya kuingia ndani ya mahakama, Jaji anaesikiliza kesi hiyo, Ahmed Refaat aliita jina la Mubaraka na rais huyo wa zamani akajibu "Nipo" kukawa na ukimya kidogo mbele ya uwepo wa wanasheria kadhaa na baadae jaji huyo akaamuru wakae chini.

Jaji huyo aliwaambia wanasheria wanatakiwa kuwa makini katika kufanikisha ufikiswaji wa maamuzi kwa umakini mkubwa. Amesema mahakama itakuwa makini na kutoa fursa kwa pande zote.

Thomas Gogis, ni mwandishi wa habari nchini Misri alisema "Kuna kitu kinaitwa haki,mahakamani, lakini kuna hukumu, vyote kwa lugha ya kiingereza vinaaza na "J" lakini hukumu inatakiwa kuwa ya haraka na haki, ni vigumu kuelewa kinachoendelea"

Nje ya mahakama hiyo kulikuwa na runinga kubwa ambapo wananchi walikuwa wakifuatilia kesi hiyo. Hata hivyo kulizuka ghasia kati ya wafuasi wa Mubaraka na kundi lingine la wanamageuzi.

" Hali imeendelea kuwa tete na hasa watu wanaonekana wakiwa wanakimbia huko na huko wakiwa wamebeba mawe, mikononi, wakibeba fimbo." alisema.

Katika kesi ya ufunguzi, kiongozi huyo wa zamani alikana mashitaka yanayomkabili likiwemo la kuamuru kuwauwa waandamanaji, walioingia mitaani kuupinga utawala wake baada ya vuguvugu la kisiasa lililozuka Januari 25.

Tuhuma za mauwaji zinazomkabili kiongozi huyo zinamuhusu pia zinamjumuisha aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani, Habib al-Adly na makamanda sita wa polisi.

Mwandishi: Sudi Mnette/ AFP
Mhariri:Josephat Charo