1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mtu mmoja auwawa mjini Narok katika machafuko ya kikabila

18 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CuGk

Mtu mmoja ameuwawa katika machafuko ya kikabilia hii leo mjini Narok karibu na mbuga ya wanyama ya Maasai Mara wakati maandamano ya wafuasi wa upinzani yalipoenea kusini mwa Kenya.

Leo ikiwa siku ya tatu na ya mwisho ya maandamano ya upinzani, polisi wamearifu kwamba mwanamume mmoja wa kabila la Kikuyu la rais Mwai Kibaki, amedungwa mkuki wa sumu wakati alipojaribu kukabilianana kundi la wamasai.

Wamasai na Wakikuyu wamekuwa wakipigana mjini Narok tangu jana huku nyumba za makaazi na maduka yakichomwa. Duru za polisi zinasema watu 23 wamejeruhiwa katika mapigano hayo.

Mzozo wa kisiasa nchini Kenya umeharibu demoraksia nchini humo, kuzitia hofu dola kuu duniani, kuwazuia watalii wasiende nchini humo na kuvuruga uchumi wa mojawapo ya nchi zilizo na uchumi imara barani Afrika.