1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Msimu mpya wa soka Ulaya kung'oa nanga

2 Agosti 2013

Msimu mpya wa kabumbu la bara la Ulaya unakaribia kuanza. Nchini Ujerumani dimba limeanza rasmi, kwa mechi za duru ya kwanza ya kombe la Shirikisho.

https://p.dw.com/p/19J2V
STUTTGART, GERMANY - APRIL 17: Players wait for the start of the DFB Cup Semi Final match between VfB Stuttgart and SC Freiburg at Mercedes-Benz Arena on April 17, 2013 in Stuttgart, Germany. (Photo by Alex Grimm/Bongarts/Getty Images)
DFB Pokal-Halbfinale VfB Stuttgart - SC FreiburgPicha: Bongarts/Getty Images

Dimba hilo linazishirikisha timu kutoka ligi kuu Bundesliga hadi za daraja ya sita..na dimba hilo halikosi mshangao. Mechi 32 zinachezwa wikendi hii. Katika dimba la mwaka jana, timu sita za Bundesliga ziliangushwa na timu za daraja za chini katika duru ya kwanza. Kile mtu anaweza kusema kwa hakika ni kuwa bila kujali ni nani atachuana na nani, kuna yule atakayeweka historia na mashabiki wa soka wa Ujerumani watapata fursa ya kujua majina mengine kadhaa mapya katika kandanda. Fainali ya dimba hilo kama kawaida huwa inaandaliwa katika uwanja wa Olimpiki mjini Berlin mwezi Mei.

Farasi wawili tena nchini Uhispania?

Nchini Uhispania, bado zimesalia wiki mbili kabla ya ligi kuu ya La Liga kuanza, na tayari huenda ikawa rahisi kutabiri ni timu zipi zitamaliza katika nafasi ya kwanza na pili. Tangu mwaka wa 2008, Barcelona na Real Madrid zimekuwa zikimaliza katika nafasi mbili za kwanza, huku Barca ikishinda mataji manne ya ligi nayo Real moja katika misimu mitano iliyopita.

Real Madrid's French defender Raphael Varane (R) celebrates after scoring during the Spanish Copa del Rey (King's Cup) semi-final first leg football match Real Madrid CF vs FC Barcelona at the Santiago Bernabeu stadium in Madrid on January 30, 2013. AFP PHOTO / PIERRE-PHILIPPE MARCOU (Photo credit should read PIERRE-PHILIPPE MARCOU/AFP/Getty Images)
Mchuano wa El Classico baina ya Barcelona na Real Madrid hutazamwa na mamilioni ya mashabiki kote ulimwenguniPicha: Getty Images

Kitu ambacho hakijulikani ni kama kocha mpya wa Real Carlo Ancelotti ataweza kubadilisha mambo, au kama kocha mpya wa Barca Gerardo Martino ataibakisha klabu hiyo kileleni. Vilabu hivyo viwili vimekuwa vikinufaika zaidi na fedha za haki ya matangazo ya televisheni kuliko vilabu vingine nchini Uhispania.

Barca na Real wawasajili nyota wapya

Wakati Barca wakiimarisha safu yao ya mashambulizi kwa kumsajili nyota wa Brazil Neymar, na wakati Real wakitarajiwa kuvunja rekodi ya uhamisho kwa kumsajili nyota wa Wales Gareth Bale, vilabu vingine vyote vimelazimika kuwauwa wachezaji wao.

Atletico Madrid, ambao walimaliza wa tatu msimu uliopita na kisha wakawashinda Real katika fainali ya kombe la Mfalme, wamemmuuza mshambuliaji wao nyota Radamel Falcao katika AS Monaco. Real Soceidad ambao walimaliza wa nne wamemuuza kiungo Asier Illaramendi katika klabu ya Real wakati nambari tano Valencia wakimuuza nahodha Roberto Soldado katika klabu ya Tottenham Hotspur.

Kuondoka kwa Soldado kuna maana kuwa wafungaji mabao mengi katika La liga msimu uliopita, Falcao, Negredo na Soldado wote wamehama ligi hiyo. Pia mshambuliaji wa Uhispania Fernando Llorente ameihama Athletic Bilbao na kujiunga na Juventus miongoni mwa wengine….

Mwandishi: Bruce Amani/DPA/AFP/reuters

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman