1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Msichana apambanaye na uhalifu

3 Desemba 2015

Msichana Sanelisiwe Dick anatayarisha na kuongoza warsha na miradi kadhaa katika eneo la Nelson Mandela Bay, akiwafikia zaidi ya wanafunzi 4,000 wa skuli za msingi na kati kwa mwaka wa tatu sasa..

https://p.dw.com/p/1HGsq
Saneliswe Dick und ihre Freunde Africa on the move Videostill
Picha: Stefan Möhl

Msichana Sanelisiwe, shujaa dhidi ya uhalifu

Sanelisiwe ni mhariri wa jarida la vijana Walmer's Own na anasimamia maktaba na pia kundi la mjadala wa kila wiki juu ya ghasia miongoni mwa vijana. Kwa msaada wa shirika moja lisilo la kiserikali, msichana huyu anaweza kutayarisha na kuongoza warsha na miradi kadhaa katika eneo la Nelson Mandela Bay, akiwafikia zaidi ya wanafunzi 4,000 wa skuli za msingi na kati kwa mwaka wa tatu sasa. Mji wa Port Elizabeth anaoishi Sanelisiwe ni wa pili kwa kuwa na ghasia nchini Afrika Kusini ambapo watu 36 kati ya laki moja huuawa kila mwaka.