1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Mripuko mwengine Irak

BAGHDAD:

Mripuko umeua watu kadhaa na kuwajeruhi wengine wengi katika Sadr City ,mashariki mwa Baghdad.Mashahidi wamearifu kuwa mripuko huo ulisababishwa na na bomu lililopangwa kuripuka pale basi la abiria liliponyemelea njia ya kuingilia Sadr city.

Ila kali zimesikika kupinga mpango wa Marekani kujenga ukuta kuzunguka eneo linalokaliwa na wairaqi wa madhehebu ya sunni mjini Baghdad.Vikosi vya Marekani vinadai ukuta huo shabaha yake ni kuilinda jamii ya wasuni walio-wachache katika wilaya ya Azamiyah iliokumbwa na machafuko .Baadhi ya wakaazi wake wameingiwa na wasi wasi na wanadai hawakushauriwa juu ya ujenzi wa ukuta huo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com