Mripuko mkubwa katika ghala ya silaha
15 Machi 2008Matangazo
TIRANA:
Mripuko mkubwa uliotokea kwenye ghala ya kijeshi umeutikisa mji mkuu wa AlbaniaTirana.Kwa mujibu wa polisi hadi watu 150 wamejeruhiwa.Mripuko huo umetokea Gerdek kiasi ya kilomita 10 kaskazini ya Tirana na ulisikika umbali wa kilomita 50 na umesababisha uharibifu katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Tirana.