Mpatanishi mkuu wa Iran katika mazungumzo ya Nuklia ajiuzulu | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 20.10.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Mpatanishi mkuu wa Iran katika mazungumzo ya Nuklia ajiuzulu

Ali Larijani amejiuzulu lakini sababu iliyochangia katika hatua hiyo haikutajwa

Ali Larijani

Ali Larijani

Msemaji wa serikali Gholam Hossein Elham amesema Ali Larijani ambaye ni katibu wa baraza kuu la usalama la Iran amejiuzulu lakini hakuna sababu zilizotolewa kutokana na uamuzi huo ingawa msemaji wa serikali amesema bwana Larijani anataka kujishughulisha na masuala mengine ya kisiasa.

Rais Mahmoud Ahmedinejad amekubali kujiuzulu kwa Larijani na naibu waziri wa mambo ya nje anayehusika na masuala ya Ulaya na Marekani Saeed Jalili ndiye atakayechukua mahala pake.

Kwa mujibu wa msemaji wa serikali wa Iran mazungumzo kati ya mjumbe wa Iran na mkuu wa sera za nje za Umoja wa ulaya Javier Solana yaliyopangiwa kufanyika jumanne yataendelea kama ilivyopangwa huko mjini Roma Italia.

 • Tarehe 20.10.2007
 • Mwandishi Saumu Mwasimba
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/C77d
 • Tarehe 20.10.2007
 • Mwandishi Saumu Mwasimba
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/C77d

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com