1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mpango mpya wa uokozi kwa ajili ya benki ya Hypo Real Estate.

Hasselmann, Silke / Berlin (HSB)6 Oktoba 2008

Serikali ya Ujerumani pamoja na taasisi za fedha zimekubali mpango wa kuinusuru benki ya mikopo ya nyumba ya Hypo Real Estate.

https://p.dw.com/p/FUlP
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na waziri wa fedha Peer Steinbrüch wakitoa taarifa katika ofisi za kansela siku ya Jumapili tarehe 05.10 ,kuhusiana na mzozo wa kifedha unaoihusisha benki ya Hypo Real Estate nchini Ujerumani.Picha: picture-alliance /dpa


Serikali ya Ujerumani pamoja na taasisi zake za fedha ikiwa ni pamoja na mabenki mbali mbali, zimekubaliana kuhusu mpango wa kuinusuru benki inayotoa mikopo ya nyumba Hypo Real Estate. Hatua hiyo inatoa uhakika kwa sekta ya fedha ya benki hiyo ya Munich kuweza kuwa na fedha za mikopo kwa kiasi cha Euro bilioni 15.


Majadiliano yalichukua saa kadha . Na kwa upande wao wawakilishi wa benki hiyo walikuwa wakivuta pumzi wakiwa na matumaini ya kundi hilo la wajumbe wa majadiliano mara hii wataweza kufanikisha, aina fulani ya uokozi , si kwa benki hiyo iliyo katika matatizo ya Hypo Real Estate bali kwa taasisi nzima ya fedha ambayo ni dhaifu nchini Ujerumani.

Pamoja na hayo waziri wa fedha wa Ujerumani Peer Steinbrüch wakati mwingi alikuwa anapinga hatua kama hiyo. Ilikuwa ni hatua muafaka kuchukuliwa kabla ya kuanza mauzo katika soko la hisa mjini Tokyo, hasa kwa kufuatia kupatikana kwa kiasi hicho cha fedha cha zaidi ya Euro bilioni 15 kwa sekta ya benki na fedha nchini Ujerumani ya kundi hili la makampuni la Hypo Real Estate.

Kitu ambacho hakikubadilika katika hali hii ni hati za dhamana za serikali.

Ililazimu kundi hilo la taasisi za fedha kuingilia kati na kutoa kiasi cha Euro bilioni 26,5 na iwapo benki ya Hypo Real Estate haitaweza kulipa deni hilo, walipakodi watagharamika kwa kiasi kama hicho kila wiki. Ndio sababu waziri wa fedha wa Ujerumani Peer Steinbrüch kwa niaba ya serikali akataka kubadili hali hiyo na kutaka kuichukua mikononi mwa serikali benki hiyo yenye matatizo.

Mwanzoni ilikuwa hali ya kutisha, kwamba viongozi wa benki hii ya Hypo Real Estate mwishoni mwa wiki hii walitaka fedha zaidi za kuendesha benki yao. Na serikali ya Ujerumani inahisi kuwa imepewa taarifa potofu kutoka viongozi wa benki hii, na kwa hiyo ninazidi kuwapa mbinyo.


Na si tu kwamba waziri ama kansela hawakupewa taarifa kamili kuhusu suala hilo, lakini pia mkuu wa benki muhimu nchini Ujerumani ya Deutsche Bank Ackermann pamoja na benki nyingine za binafsi hawakuchukua hatua madhubuti za kudhibiti hali hii , sababu ikiwa ni kutokana na taarifa mpya juu ya kupanda kwa gharama za mpango wa kwanza wa kuinusuru benki hiyo. Ndio sababu kila kitu kilisambaratika mwanzoni na ikabidi kuanza upya majadiliano. Na ndipo kansela Merkel akasema wazi kuwa.

Hatutaweza kuachia , hali hii mbaya ya taasisi moja ya fedha iharibu utaratibu wote wa taasisi nyingine za fedha.


Wakati huo huo mawaziri wa fedha wa mataifa ya umoja wa Ulaya wanakabiliwa na mbinyo mkali leo Jumatatu na kesho Jumanne kuweza kupata dawa ya kudhibiti mzozo huu ulioanzia huko Marekani wa fedha ambao hivi sasa unasambaa kama moto katika mataifa ya Ulaya, huku wazo la mtindo wa kunusuru taasisi za fedha kama ilivyofanya Marekani likijitokeza tena. Katika mkutano wa dharura uliofanyika mjini Paris mwishoni mwa Juma, viongozi wa Uingereza, Ufaransa, Ujerumani na Itali waliahidi kulinda benki zilizodhaifu, lakini walitupilia mbali uwezekano wa kuunda mfuko wa pamoja wa Ulaya kunusuru mabenki.

Saa 24 baadaye waziri mkuu wa Itali Silvio Berlusconi amesema kuwa anataka kuufufua mpango huo.

►◄