1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahanga wapokea misaada

Mazula, Scholastika22 Januari 2008

Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa, WFP limeanza zoezi la kusambaza chakula na kuweka makazi kwa waathirika wa mafuriko nchini Msumbiji.Kiasi cha tani mbili nukta mbili za vyandalua, mahema na vifaa vingin

https://p.dw.com/p/Cw9T
Maporomoko ya maji MsumbijiPicha: DW



Kwa mujibu wa WFP; awamu ya kwanza ya chakula ilitarajiwa kuwasilishwa jana katika eneo la Goligoli ambako kiasi cha watu elfu kumi na tatu wameyahama makazi yao kutokana na mafuriko.


Shirika la Mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa linatarajia kusambaza tani sabini na nne za chakula katika Mji wa Goligoli ambazozitasafirishwa na helkopta kwa muda wa siku nne ama tano.



Asilimia kubwa ya waathirika wa mafuriko hayo, wako katika maeneo ambayo hayapitiki kwa sababu hakuna barabara za kuweza kufika maeneo hayo kama vile katika majimbo ya Tete, Sofara na Manica.


Hata hivyo Umoja wa Mataifa umeanza kusambaza msaada wa haraka wa chakula  kwa njia ya barabara.


Kabla ya mafuriko mabaya kutokea, WFP;ilikuwa ikitoa msaada kwa watu laki moja na tisini elffu ambao walipoteza mazao yao kutokana na mafuriko ya Zambezi yaliyotokea mwaka jana.


Taasisi ya kitaifa inayoshughulika na mambo ya majanga, mapema juma lililopita ilisema kwamba mafuriko yanayotokea hivi sasa nchini Msumbiji yataleta hasara kubwa zaidi ya yale yaliyotokea mwaka 2000 hadi 2001 yaliyosababishwa na mvua iliyonyesha kwa kipindi kirefu nchini humo  bila kukatika na kuharibu zaidi ya makazi mia saba.


Tangu kuanza kwa kipindi cha Mvua mwezi Novemba mwaka jana, Mvua kubwa zimesababisha kuongezeka kwa kasi kwa kina cha maji katika mito ya Zambezi, Pongue, Buzi na save katika eneo la kati na kusini mwa nchi hiyo.


Zaidi ya watu elfu sabini wamehamishiwa hasa katika mashule na majengo mengine ya Serikali.


 Wakati huo huo shirika la misaada la Kimataifa la Hispania linalojulikana kama AECI; limesema kwamba limetoa msaada kiasi cha euro milioni moja nukta mbili ssawa na dola milioni moja nukta nane kwa ajili ya kusaidia Nchini Kenya ambako kunamachafuko ya Kisiasa na kuisaidia nchi ya Msumbiji ambayo imekumbwa na mafuriko. 


  AECI; imesema kuwa inakusanya tena kiasi cha euro laki saba na thelathini na tano kwa ajili ya Msumbiji ambako mafuriko yameua kiasi cha watu kumi na wengine hamsini na tano elfu wameyakimbia makazi yao kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Serikali ya Msumbiji.


fedha hizo zitasaidia kununua nafaka za vyakula ili ziweze kuwasaidia watu wapatao laki mbili na themanini katika kipindi ccha siku kumi na tano ikiwa ni pamoja na kununua matunubari, maji ya akiba na nyingine zitagharamia usafiri wa helkopita wakati wa usambazaji wa misaaa hiyo.


Mapema wiki iliyopita Shirika la Kimataifa la msalaba mwekundu lilitangaza kuomba msaada wa euro milioni tano msaada wa Kimataifa ili kuzisaidia nchi za Msumbiji, Zambia na Zimbabwe zilizokumbwa na mafuriko.


Aidha kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa jana na Serikali ya Msumbiji, mbaka sasa mafuriko hayo yameua watu kumi na nne na na kuifanya Serikali ya nchi hiyo kuhitaji msaada wa dola milioni arobaini na tatu ili kuendeleza zoezi la utoaji wa huduma za kiutu.


mafuriko yanayozikumba nchi za Zambia, Msumbiji, Zimbabwe na Malawi yametokana na mvua kubwa iliyonyesha mfululizo kwa kipindi cha wiki kadhaa nakusababisha mauaji ya watu na wengine yalazimishwa kuvihama vijiji vyao.





►◄