Je Msumbiji imekuwa mno kuwa jamii ya asasi zisizo za kiserikali?
12 Julai 2008
►◄
Vyama vya kijamii, au asasi zisizo za kiserikali nchini Msumbiji ni dhaifu, inaeleza ripoti moja juu ya hali ya asasi hizo nchini humo iliyotolewa mapema mwaka huu.
Hii inathibitisha tu ukweli ambao uko wazi, kuhusiana na asasi za kijamii katika kupambana na umasikini, katika hilo kwa kiasi kikubwa asasi hizo zinakuwa ni watazamaji tu na wasikilizaji.
Ripoti hiyo ambayo imepewa kichwa cha habari , kielelezo cha vyama vya kijamii nchini Msumbiji 2007, imegundua kuwa athari za asasi za kijamii katika jamii ya nchi hiyo zinaukomo; kusajili asasi kama hizo ni kazi ngumu kutokana na urasimu uliopita kiasi, na vyama ambavyo vipo vinapata taabu ya kuhakikisha vinatimiza sheria zilizopo na kwa kiasi kikubwa zinawekwa kando katika mchakato wa kisiasa, na mara kadha hazitekelezi maadili ya kidemokrasi na uwazi ambayo zinapigia upatu.
Paulo Cuinica, katibu mkuu wa G20, chombo kinachojumuisha asasi zaidi ya 400 pamoja na mitandao iliyoanzishwa 2003, anakiri udhaifu katika sekta hiyo, lakini anasisitiza kuwa vyama hivyo vya kijamii vimekuwa vikipata nguvu kila uchao hivi karibuni na hususan viko hai katika maendeleo ya nchi hiyo.
Katika mwaka 2004, tumetoa ripoti ya umasikini ambayo ilitoa mchango fulani ambao serikali taratibu inauingiza katika sera zake, kama vile mabaraza ya wilaya ya ushauri amesema.
Mabaraza ya ushauri ni vyombo vinavyojumuisha vyama vya kijamii na taasisi za serikali , ambayo huchukua maamuzi kwa niaba ya wilaya kuhusiana na mipango na utaratibu wa utekelezaji katika hatua zinazoendelea za kutoa madaraka mikoani.
Katika kuendeleza hilo, kundi la G20 pia limeshiriki katika ushauri wa mwaka 2005 pamoja na hatua za usambazaji wa waraka wa taifa wa mkakati wa upunguzaji umasikini, unaofahamika kama PARPA ll.
Vingi ya vitu muhimu vilitumika , amesema Cuinica , lakini anadokeza kuwa changamoto kwa vyama vya kijamii ni kuona kuwa sera hizo zinatafsiriwa kuwa vitendo.
Na ni katika hatua ya utekelezaji ndipo asasi za kijamii nchini Msumbiji zinakosa kwa kiasi kikubwa uwezo wa kujadili kwa kiwango kile kile na wafadhili pamoja na serikali.
Tunapaswa kuongeza uwezo wetu wa kutathmini ama inawezekana kuwapo na hatari ya mikutano kama hiyo kuwa haina maana.
Tangu mwaka 2004, kundi la G20 limeshiriki katika uchunguzi wa hali ya umasikini ambao ni baraza la majadiliano baina ya serikali , wafadhili na vyama vya kijamii kuhusu muundo na mwelekeo wa sera za kijamii na kiuchumi za nchi. Ushiriki wa vyama vya kijamii vya Msumbiji katika baraza hilo la uchunguzi umesifiwa kuwa ni mafanikio, na kwa kiasi kwamba katika mkutano wa kimataifa wa ushauri juu ya umasikini na maendeleo uliofanyika nchini Mauritius mwezi wa Aprili, jumuiya ya kiuchumi ya nchi za kusini mwa Afrika SADC iliamua kuunda baraza kama hilo la kieneo kuangalia hali ya umasikini.
Mkutano huo wa Mauritius pia ulikuwa ni mara ya kwanza kwa vyama vya kijamii kualikwa kushiriki katika mkutano wa SADC.