1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MOSUL:Viongozi wa kidini wauwawa Iraq

Wanamgambo wanaendelea kufanya mashambulio mjini Mosul licha ya kuwepo opresheni za wanajeshi wa Marekani na Iraqi.

Mashambulio hayo yanawalenga hasa viongozi wa kidini katika mji huo wa tatu kwa ukubwa nchini Iraq.

Hapo jana viongozi watatu wakidini wa madhehebu ya wasuni waliuwawa na watu waliokuwa na silaha.Sheikh Ghanem ambaye ni Imamu wa msikiti wa Al sadiqi alipigwa risasi hapo jana nje ya nyumba yake kusini mwa Mosul wakati Sheikh Salem Sheet alipigwa risasi nje ya msikiti anakosalia wa AL Sahaba.Na imamu wa tatu Sheikh Azkher Ahmed Hussein aliuwawa na watu wasiojulikana katika tukio tofauti nje ya nyumba yake huko mashariki mwa mji huo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com