1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Mosul.Shambulio la kujitoa muhanga lafanywa huko Mosul.

Mshambuliaji wa kujitolea muhanga akiwa katika gari la mafuta amijiripua karibu na kituo cha polisi katika mji wa Mosul nchini Iraq na kupelekea kuuwawa kwa watu saba na kuwajeruhi wengine 20, wengi wao wakiwa polisi.

Vyanzo vya habari vya hospitali vimesema, idadi ya vifo inaweza ikaongezeka, lakini hakukuwa na taarifa zaidi.

Mripuko huo uliokuwa mkubwa, ulisikika katika mji wote wa Mosul kilomita 390, kaskazini mwa Baghdad.

Mji wa Mosul hadi hivi sasa umeshashuhudia mara kadhaa umwagaji wa damu, tangu pale Wasunni walipovishambulia vikosi vya kijeshi vya Marekani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com