MOSKOW.Urusi yahofia meli yake kuwa imezama | Habari za Ulimwengu | DW | 24.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MOSKOW.Urusi yahofia meli yake kuwa imezama

Utawala nchini Urusi unahofia kuwa meli iliyokuwa na shehena ya mbao iliyo kuwa ikielekea China huenda ikawa imezama baada ya kukumbwa na dhoruba kali katika pwani ya Japan.

Habari zaidi zinafahamisha kuwa hali ya mabaharia 18 waliokuwa ndani ya meli hiyo kwa jina Sinegorye haijulikani.

Maafisa mjini Moskow wameeleza kuwa nahodha wa meli hiyo alituma ujumbe wa kuomba msaada baada ya kugundua kuwa matanga ya meli hiyo yameharibiwa na shehena iliyokuwa ikiporomoka ovyo.

Meli hiyo baadae iliambaa kuelekea pwani ya Korea Kaskazini kabla ya kupoteza mawasiliano.

Vyombo vya habari vya Urusi vimesema kuwa meli hiyo ilikuwa kilomita 120 umbali na ghuba ya Korea Kaskazini wakati wa ajali hiyo.

Manowari 20 zimekwenda katika eneo la ajali lakini hali mbaya ya hewa na mawimbi makubwa yanatatiza shughuli za uokozi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com