1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW : Watuhumiwa kutorudishwa Uingereza

6 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCm5

Mwendesha mashtaka mkuu wa serikali nchini Urusi hatowarudisha nchini Uingereza watuhumiwa wa kifo cha Alexander Litvinenko kutokana na kupewa sumu.

Lakini mwendesha mashataka huyo Yuri Chaika amesema kwamba Urusi itatowa ushirikiano wake kwa wapepelezi wa Uingereza ambao hivi sasa wako mjini Moscow kukusanya ushahidi juu ya kifo mjini London cha mpelelezi huyo wa zamani wa Urusi. Madaktari waligunduwa polonium 210 sumu ya miale ya nuklea ya aina yake kwenye mwili wa Litvinenko kabla kufa kwake hapo Novemba 23.

Serikali ya Urusi imekanusha madai kwamba imehusika na mauaji ya Litvinenko ambaye alikuwa mkosoaji mkali wa Rais Valdimir Putin wa Urusi.