MOSCOW: Watu 36 wauawa katika ajali ya mgodi Russia. | Habari za Ulimwengu | DW | 24.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MOSCOW: Watu 36 wauawa katika ajali ya mgodi Russia.

Watu thelathini na sita wameuawa na wengi kama ishirini wamenaswa chini ya ardhi baada ya mlipuko mkubwa kutokea kwenye mgodi wa makaa ya mawe katika eneo la Kemerovo, Siberia nchini Russia.

Kiasi wachimba migodi mia moja na themanini waliondolewa mahali hapo punde baada ya tukio hilo.

Mwezi Machi, mgodi wa karibu na mahali hapo ulilipuka na kusababisha vifo vya watu zaidi ya mia moja.

Migodi ya makaa ya mawe ya Russia mara kwa mara hukumbwa na ajali ambazo zinasemekana zinatokana na mitambo ya zamani na pia upungufu wa kuwekeza kwenye sekta ya madini hayo tangu Urusi ya zamani iliposambaratika.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com