MOSCOW: Waandamanaji wapata kipigo | Habari za Ulimwengu | DW | 28.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MOSCOW: Waandamanaji wapata kipigo

Wafuasi wa kanisa la Orthox wenye msimao mkalai wa kidini wamewashambulia na kuwapiga waandamanaji wanaopigania haki za wasenge waliokuwa wakiandamana mjini Moscow nchini Urusi.

Polisi waliwazuilia kwa muda wabunge wawili kutoka Ulaya waliokuwa wakizuru mjini humo, akiwemo mwanachama wa chama cha Kijani hapa Ujerumani, Volker Beck.

Watetezi 30 wa haki za wasenge walikamatwa na polisi ambao walisimama na kutazama jinsi waandamanaji mjini Moscow walivyoshambuliwa wakati wa maandamano yao ambayo hayakuidhinishwa.

Waandamanaji hao walitaka kuwasilisha ombi kwa meya wa mji wa Moscow wakidai haki ya kufanya maandamano.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com