1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW: Viongozi watoa heshima zao kwa marehemu Yeltsin

24 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC7Y

Viongozi mbalimblai duniani kote wameungana na rais wa Urusi Vladamir Putin kutoa heshima zao za mwisho kwa rais wa zamani wa nchi hiyo, Boris Yeltsin aliyefariki dunia jana akiwa na umri wa miaka 76.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amesema Yeltsin atakumbukwa kwa jukumu lake katika kuendeleza mageuzi ya kisiasa na kiuchumi nchini Urusi.

Kansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel, amesema Boris Yeltsin alipigania demokrasia na uhuru na alikuwa rafiki wa dhati wa Ujerumani.

Rais wa Korea Kusini Roh Moo- Hyun leo amemsifu marehemu Boris Yeltsin kwa kudumisha uhusiano wa kirafiki baina ya Urusi na Korea Kusini.

Mazishi ya marehemu Yeltsin yamepangwa kufanyika kesho. Rais Vladimir Putin ametangaza kesho kuwa siku ya maombolezo ya kitaifa.

Marehemu Boris Yeltsin alichukua hatamu za uongozi kama rais wa Urusi baada ya kuchaguliwa kwa njia ya kidemokrasia mnamo mwaka wa 1991 na akashikilia wadhifa huo hadi alipojiuzulu mnamo mwaka wa 1999.

Aliiongoza Urusi kuwa soko la kiuchumi lakini pia akaanzisha ita vibaya dhidi ya waasi waliojitenga wa Chechnya mnamo mwaka wa 1994.