1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW: Urusi yataka Georgia iondoe majeshi yake Abkhazia

4 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD6R

Urusi inatafuta msaada wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuilazimisha Georgia iwaondoe wanajeshi wake kutoka eneo lililo karibu na jimbo lililojitenga la Abkhazia.

Wanadiplomasia wa Urusi wamewasilisha azimio wakiihimiza Georgia iondoke kutoka bonde la Kodori, eneo linaloiunga mkono Urusi, na ifutilie mbali mpango wake wa kuanzisha serikali mpya katika eneo hilo.

Pendekezo hilo limetolewa wakati kukiwa na hali ya wasiwasi kati ya Georgia na Urusi kufuatia kisa cha kukamatwa na kuachiliwa huru kwa wanajeshi wa Urusi walioshukiwa kuwa makachero na maofisa wa usalama wa Georgia.